
SERA YA TAIFA YA MAENDELEO YA VIJANA YA MWAKA 2007
Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana (2007), Toleo la Mwaka 2024, inajengwa juu ya mafanikio ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana (2007) ikiwa na lengo la kushughulikia mazingira yanayoendelea kubadilika ambayo vijana wa Tanzania wanakabiliana nayo. Kwa kutambua changamoto na fursa muhimu zinazoletwa na ulimwengu unaobadilika kwa kasi, Sera hii inaainisha mfumo kamili na madhubuti wa kuwawezesha na kuwaendeleza vijana kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Toleo hili linaendana na mabadiliko ya kidijitali, kuwawezesha vijana kuwa na ujuzi na maarifa stahiki ili kushiriki kikamilifu katika ulimwengu wa teknolojia. Aidha, Toleo hili linashughulikia masuala muhimu kama vile kushuka kwa maadili, changamoto za kiafya na lishe, na ufinyu wa fursa za uongozi kwa vijana. Sera hii pia inalenga kuwawezesha vijana wa Kitanzania kutumia uwezo na vipawa vyao kukuza na kuimarisha utamaduni wa uvumbuzi, ujasiriamali, uzalendo na utaifa.
Read more: …. https://d5c99pbctona6.cloudfront.net/PZtPN79QV58gVdeWubyAgBUsQQDzc1kBP5tr15foQL4q7acjEopxGYqZxJ9E0cRw.pdf
- Written by DDA Hub Admin
- Created Date May 07, 2025