
DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050
Katika kujiwekea mipango thabiti ya maendeleo, mwaka 2000 Tanzania ilizindua Dira ya
Taifa ya Maendeleo 2025, ambayo ililenga kulijenga taifa kuwa nchi ya kipato cha kati.
Maeneo ya kipaumbele yalikuwa ni kilimo cha kisasa, viwanda, miundombinu, na
teknolojia. Dira 2025 imeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watu, ukuaji wa
uchumi, na utawala, huku kukiwa na ongezeko la ushiriki wa wanawake katika siasa na
uchumi.
Tangu kuzinduliwa mwaka 2000, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 imekuwa nyenzo
muhimu katika kusukuma mbele maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.
Msingi wa mafanikio haya umejengwa juu ya misingi ya amani, utulivu na umoja wa
kitaifa, hali iliyowezesha utekelezaji wa sera, kuvutia uwekezaji, na kuimarisha
mshikamano wa kitaifa.
https://cdn.sanity.io/files/9tk5hdku/production/80e3bc999bea6d0d196f5dec5b19c6aef77fe9bf.pdf
- Written by DDA Hub Admin
- Created Date Jul 26, 2025